Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amesaini kitabu cha Waombolezaji nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Ismani Marehemu Mhe. William Vangimembe Lukuvi, Mwili wa Mhe. Lukuvi utawasili leo Mkoani Iringa ukitokea Dar es Salaam baada ya Wananchi wa Dodoma na Dar es Salaam kupata fursa ya kuaga.
Mhe. Lukuvi alifariki Dunia tarehe 25 Machi, 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Benjamin Mkapa.




No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇