LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 12, 2026

SHANGWE ZARINDIMA NAIBU WAZIRI MWINJUMA AKITANGAZA KUSHUSHA ADA ZA LESENI ZA MITANDAO YA HABARI

 SERIKALI kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TBA), imepunguza ada za leseni kwa Wanablogu na wakusanyaji wa maudhui (Online Content Aggregators).

Punguzo hilo limetangazwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC) Februari 12, 2026 jijini Dodoma.

Aidha, kundi la "Amateur" limeanzishwa kwa ajili ya vijana wanaochipukia 

Naibu Waziri Mwinjuma amesema kuwa ada ya leseni ya 'wakusanyaji maudhui mtandaoni imepunguzwa kutoka sh. 1,000,000 hadi Sh. 100,000 kwa mwaka na fomu ya usajili imepungua kutoka 100,000 hadi sh. 20,000. Ada ya leseni ya blogu imepungua kutoka sh. 500,000 hadi sh. 50,000 kwa mwaka  na fomu ya usajili imetoka sh. 50,000 hadi sh. 10,000.

Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa kina na mikutano ya kimkakati ya takribani mwaka mzima kati ya mtandao wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikielezea vikwazo vya gharama vilivyokuwa vikikwaza uandishi wa habari za kidijitali nchini.

Awali katika mkutano huo, Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Andrew Kisaka ya  alitangaza nafuu ya kutolipa ada kwa mwaka mmoja kwa waandishi wa habari wanaoanzisha mitandao ya habari watakao tambulika kama 'ameteur'ili waweze kujitambulisha rasmi na kukuza vipaji vyao bila vikwazo vya kifedha.


Awali anayetaka kuanzisha mtandao wa habari alitakiwa alipe ada ya maombi sh. 50,000 na ada ya leseni sh. 500,000 kwa mwaka.

Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na wamiliki wa mitandao waliohudhuria mkutano huo ambao baada ya Naibu Waziri Mwinjuma kutangaza walishangilia kwa kupiga makofi. 

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku mbili ni wanachama wa Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN), Jumuiya ya  Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), MOAT, NIBA, Wakongwe RTD, Baraza la Habari Tanzania (MCT), MISA Tanzania na EACO.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages