LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 22, 2026

RAIS SAMIA ANATAMANI KUONA TABASAMU LA WATU WA CHINI, TWENDE TUKAGUSE MAISHA YAO- DKT. MAJULE

 Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Majule (katikati) ametoa msaada wa vyakula, vinywaji, vifaa vya usafi na vyandarua 100 kwa Shule ya Viziwi Dodoma, katika tukio lililofanyika Februari 21, 2026 katika shule hiyo iliyopo Kisasa jijini Dodoma.

Katika tukio hilo, Dkt. Majule ambaye yupo mstari wa mbele kujitotea kwa hali na mali katika masuala ya kijamii na hasa kwa watu wenye uhitaji maalumu, alitoa mchele, unga, mafuta, sukari, vinywaji, sabuni, fagio, kalamu, madaftari na pedi kwa ajili ya mabinti. Kabla ya makabidhiano ya msaada huo, Dkt. Majule alipata wasaa wa kutembelea na kujionea jinsi wanafunzi wanavyopata mafunzo kwa njia ya vitendo ikiwemo ushonaji, kompyuta, ufundi umeme na uselemala lakini pia mchezo wa pooltable. Mkuu wa shule hiyo, Awadhi Mbogo alitoa shukrani kwa kitendo cha mbunge huyo kuamua kutoa msaada huo mkubwa kwa shule hiyo na kwa aendelee na moyo huo wa kujitolea na kutoa wito kwa wananchi wengine kuiga mfano huo. Akizungumza katika tukio hilo, Dkt. Majule amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan akilihutumia Bunge Novemba 14, 2025, alisema anatamani kuona Tabasamu la watu wa Chini kabisa, hivyo inatakiwa "tumuunge mkono kwa kutoa misaada kwa watu hao na hasa wenye uhitaji maalumu." Aidha, Dkt. Majule amesema kuwa baada ya kufanikiwa kupata ubunge sadaka yake ya kwanza ameamua kuipeleka katika shule hiyo ya viziwi Dodoma. Shule hiyo ambayo ni ya serikali, chini ya Manispaa ya Dodoma inasimamiwa pia kwa msaada wa Robin Donker Sgoed ambaye ni Mwasisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Environmental Oriented and Training Support (EOTAS).

Dkt. Majule akikabidhi vyakula.


Dkt. Majule akigawa vyandarua hivyo kwa wanafunzi.


Madaftari.
 
Vifaa vya usafi.


Dkt. Majule akigawa vinywaji.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Dodoma, Zainab Mtoro akisaidia kugawa vinywaji.


Wanafunzi wakifurahia vinywaji hivyo.
Wanafunzi wa darasa la kompyuta.


Dkt. Majule akiwaaga wanafunzi.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA- 0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages