LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 13, 2026

RAIS SAMIA AHUDHURIA MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIANCHI AFRIKA CAHOSCC 2026


RAIS Dk Samia Suluhu Hassan akiwasili katika jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC) wa mwaka 2026, Februari 13, 2026, jijini Addis Ababa, Ethiopia, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, Dk William Ruto.


Kikao hiki muhimu, kinachofanyika kuelekea Mkutano wa 39 wa Umoja wa Afrika (Februari 14-15), kinalenga kuharakisha hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha msimamo wa pamoja wa Afrika katika suala zima la mabadiliko ya tabia nchi.








 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages