Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu John Mongella, amesikiliza kero na maoni ya mabalozi kutoka Wilaya za Ilemela na Nyamagana, katika mkutano uliofanyika leo tarehe 04 Februari, 2026, katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Mwanza.
Akizungumza katika mkutano huo, Mongella aliwapongeza Mabalozi kwa michango na maoni yao mazuri ya kukijenga Chama kuanzia ngazi ya Shina, huku akisisitiza umuhimu wa Mshikamano, Uwajibikaji na Uadilifu katika utekelezaji wa majukumu ya Chama katika maeneo yao.
Aidha, Mongella aliahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na Mabalozi, ikiwemo kuwawezesha vitendea kazi kwa Mabalozi ili waweze kuwa na ufanisi katika utendaji kazi wao na kuimarisha mawasiliano na Wanachama.
Mkutano huo umefanyika katika hali ya utulivu na mshikamano, ukiakisi dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ya kusikiliza maoni ya Wanachama wake na kuendelea kusonga mbele kwa Umoja na Amani.
“Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.”

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇