LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 24, 2026

KATIBU WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM, STANLEY MKANDAWILE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KIFO CHA POLYCARP PENGO, ATOA NENO.

 đź“ŤSt Joseph 
📆 24 February 2026 

Na CCM Blog, St Joseph, Dar es Salaam, leo
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire  leo Jumanne, Februari 24, 2026, amefika kutoa pole na kusaini Kitabu cha Maombolezo, kufuatia kifo cha Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, kilichotokea usiku wa Februari 19, 2026, katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Mkandawile katika msafara wake aliambatana na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga ambaye pia alipata fursa ya kusaini kitabu cha maombolezo, na walipokewa na Paroko wa Kanisa Kuu hilo Padri Denis Wigira Ofisini kwake na kuwa na mazungumzo mafupi, kabla ya kwenda kusaini kitabu hicho cha maombolezo. 

Akizungumza baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Mkandawile alitoa salam za pole za rambirambi kwa niaba ya CCM mkoa, akisema CCM mkoa huo ilipokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Polycarp Pengo, na kwamba wana CCM wanamkumbuka Kardinali Pengo kama kiongozi wa kiroho na mzalendo aliyetoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani, maadili, umoja na mshikamano wa kitaifa, kupitia uongozi wake wa muda mrefu ndani ya Kanisa Katoliki.

Amesema, Wana CCM na Taifa kwa jumla wamepoteza kiongozi aliyelitumikia kwa uadilifu na kujitolea, na kwamba mchango wake katika malezi ya kiroho na maadili utaendelea kukumbukwa, kuthaminiwa na kuenziwa.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Polycarp Pengo atazikwa Jumamosi, Februari 28, 2026 katika Pugu Pilgrimage Centre, nje ya Dar es Salaam,  Kaburi lake la milele litakuwa hapo alipopendelea awezikwe, kama alivyokuwa ametoa matakwa yake kabla ya kifo.

Kabla ya mazishi, Ijumaa, Februari 27, 2026, mwili wake utakuwa St Joseph’s Cathedral kuanzia asubuhi mapema kabla ya kuhamishwa hadi Pugu kwa mazishi siku iliyofuata.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akisaini leo, Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, kilichotokea usiku wa Februari 19, 2026, katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akiendelea kusaini leo, Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, kilichotokea usiku wa Februari 19, 2026, katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akitoa heshima baada ya kusaini leo, Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, kilichotokea usiku wa Februari 19, 2026, katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga, akisaini leo, Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, kilichotokea usiku wa Februari 19, 2026, katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akizungumza na Paroko wa Kanisa Kuu hilo Padri Denis Wigira baada ya kusaini kitabu hicho. Kushoto ni Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga,
Wakiendelea na mazungumzo.
Wakiendelea na mazungumza kabla ya kuagana.
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stanley Mkandawile na Mwenezi mkoa Ally Bananga wakisindikizwa na Padri Denis Wigira wakati wakiondoka baada ya kusaini kitabu hicho.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages