LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 8, 2026

DKT. KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA AFYA ESWATINI



Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, anashiriki Mkutano wa 67 wa Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (ECSA-HC) unaofanyika Ezulwini, katika Falme ya Eswatini. 


Katika hotuba yake ya ufunguzi umuhimu wa nchi wanachama kubuni vyanzo endelevu vya ndani vya kugharamia afya huku akitaja mafanikio ya Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan na mchango wa mpango wa Jamii Salama wa JMKF katika kufikia akina mama wajawazito maeneo ya vijijini Tabora.

Pembeni mwa mkutano, Dkt. Kikwete aliongoza wajumbe kumtembelea Mfalme Mswati III, ambaye ameahidi kupokea na kuwasilisha mapendekezo ya mkutano kwa viongozi wenzia wa kanda hiyo.







 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages