Zaidi ya waandishi wa habari 3200 kati ya 3900 walioomba vitambulisho vya uandishi wa habari (Press Card) baada ya kuthibitishwa na Bodi ya Ithibati ya Waadishi wa habari (JAB).
Tarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Ithibati kwa watangazaji na waandishi wa habari katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC) Februari 13, 2026 jijini Dodoma.
Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana na kufunguliwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo ni wanachama wa Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN), Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), MOAT, NIBA, Wakongwe RTD, Baraza la Habari Tanzania (MCT), MISA Tanzania na EACO.








No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇