Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Rhimo Nyansaho akutana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini ndugu Lentz Dodoma.
Akiwa jijini Dodoma, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Lentz amekutana kwa mara ya kwanza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Rhimo Nyansaho.
Mazungumzo yao yalilenga katika kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi kati ya Marekani na Tanzania, ambapo pande zote mbili zilionesha matumaini na shauku kubwa kwa mazoezi yajayo ya pamoja ya kijeshi kama hatua muhimu ya kuendeleza uimara na utayari wa vikosi, weledi, na ushirikiano wa muda mrefu wa kiusalama — jitihada zinazosaidia kuzifanya Tanzania na Marekani kuwa salama.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇