Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani itakayotekelezwa kwa siku 60 nchi nzima.
Prof. Mkumbo amewahimiza wananchi wanaomiliki ardhi kuacha kuihifadhi bila matumizi na badala yake kuitumia katika shughuli za uzalishaji ili iwe chanzo cha kipato na kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa taifa.
Amesisitiza kuwa kumiliki ardhi pekee bila mtaji, teknolojia au ushirikiano wa kibiashara hakumnufaishi mmiliki wala taifa, hivyo akashauri wananchi kuitumia TISEZA kuwatafutia wabia sahihi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri, amesema mamlaka hiyo imejiwekea lengo la kuvutia na kusajili miradi isiyopungua 1,500 katika kipindi kijacho.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇