LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 2, 2025

SERIKALI HAIPO TAYARI KUAMRISHWA, KUPEWA MASHARTI AU KULEKEZWA



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻, amesema Serikali anayoiongoza ya awamu ya sita si serikali ya kuamrishwa, kupewa masharti, au kuelekezwa namna ya kuendesha majadiliano na wadau mbalimbali wa mambo ya kisiasa.


Rais Dkt. Samia amesisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru linalojiongoza kwa misingi ya mamlaka yake kamili na si kundi la watu linaloweza kushinikizwa.

Akilihutubia Taifa kupitia mkutano wake na Wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo  Disemba 2, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC.

  Rais Samia, amesema kumekuwapo na taarifa za baadhi ya makundi ya kisiasa na watu wanaoendelea kutoa masharti kabla ya kukubali kukaa meza moja kufanya mazungumzo, ikiwamo masharti ya “mfanye hili”, “mwachie huyu”, au “tekelezeni kigezo hiki kabla ya kuzungumza.”

"..wanadamu hukosana na wakaelewana...inawezekana kabisa kuna mapungufu na hakuna serikali yoyote duniani isiyo na mapungufu lakini wanakaa, wanazungumza na kuondoa mapungufu yaliyopo."

Kwa msisitizo, Rais Dkt. Samia “Serikali hii si ya kuamrishwa wala kupewa maelekezo,”

Aidha, Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa mazungumzo yanayokusudiwa ni yale ya kuheshimiana na kutambua nafasi ya kila upande.


 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages