LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 12, 2025

RAIS DKT. MWINYI AKABIDHIWA RASMI TUZO YA "AFRICAN'S BEST CORPORATE RETREAT DESTINATION 2025"

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 12 Desemba 2025, amepokea tuzo ya kuwa Kivutio Bora cha Mikutano ya Kimkakati Barani Afrika (African’s Best Corporate Retreat Destination 2025). Tuzo hiyo imetolewa baada ya Zanzibar kushinda katika Tuzo za Utalii Duniani (World Travel Awards 2025) zilizofanyika nchini Bahrain.

Mhe. Rais Mwinyi amekabidhiwa tuzo hiyo Ikulu Zanzibar na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), kama ishara ya kutambua mchango na mafanikio makubwa ya Zanzibar katika kukuza sekta ya utalii wa mikutano na matukio ya kimkakati. Ushindi huu umeiweka Zanzibar katika ramani ya dunia baada ya kuibuka kinara dhidi ya mataifa mengine yaliyokuwa yakishindanishwa.

Tuzo hii inaendelea kuthibitisha mageuzi makubwa yanayoendelea katika sekta ya utalii, sambamba na jitihada za Serikali ya Zanzibar kuboresha miundombinu, huduma na mazingira rafiki kwa uwekezaji na mikutano ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages