Jeshi la Polisi Tanzania limesema linaendelea kumtafuta Augustino Polepole aliyejitambulisha kuwa ni Ndugu wa Humphrey Polepole ili aweze kulipa Jeshi hilo ushirikiano na kutoa maelezo yake na uthibitisho wa shutuma alizotoa kwamba Afisa wa Jeshi la Polisi alihusika kumteka Polepole.
Taarifa ya leo Oktoba 07, 2025 iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo, Makao Makuu ya Polisi, Dodoma imeeleza kuwa kama lilivyotoa taarifa yake jana Oktoba 6, 2025, kwamba Jeshi hilo limeanza uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa na Augustino Polepole kuwa, Ndugu yao Humphrey Polepole ametekwa na jalada la uchunguzi lilifunguliwa jana hiyo hiyo.
“Pamoja na kukusanya taarifa mbalimbali, Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Augustino Polepole ili aweze kutupa ushirikiano na kutoa maelezo yake na uthibitisho wa shutuma alizotoa kwamba, Afisa wa Jeshi la Polisi alihusika katika tukio alilolitolea taarifa kupitia mitandao ya kijamii”, imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi amesema, hiyo inaenda sanjari na kututhibitishia kuwa Humphrey Polepole alikuwa ni mpangaji au mkazi wa nyumba aliyodai kuwa utekaji ulifanyika.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇