𝘼𝙨𝙚𝙢𝙖 𝘿𝙖𝙧 𝙚𝙨 𝙨𝙖𝙡𝙖𝙖𝙢 𝙞𝙢𝙚𝙬𝙖𝙘𝙝𝙖𝙥𝙖 𝙫𝙞𝙗𝙤𝙠𝙤 𝙢𝙖𝙟𝙞𝙧𝙖𝙣𝙞 𝙠𝙬𝙖 𝙪𝙢𝙖𝙩𝙞 𝙪𝙡𝙞𝙤𝙟𝙞𝙩𝙤𝙠𝙚𝙯𝙖 𝙇𝙚𝙖𝙙𝙚𝙧𝙨 𝘾𝙡𝙪𝙗
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu. Kenani Kihongosi amesema kuwa ujio wa maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Kinondoni na Ubungo katika viwanja vya Leaders Club ni jibu tosha la kukubalika kwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM na Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻.
Mwenezi Kenani ameyasema hayo leo tarehe 21 Oktoba 2025 mbele ya wananchi wa Majimbo ya Kinondoni, Ubungo, Kawe na Kibamba ambao kwa kauli moja wamekubaliana na alichokisema na kuongezea kuwa wametoka kwao kumfata SAMIA ili kumthibitishia ushindi wa kutosha ifikapo Oktoba 29.
Aidha, Mwenezi Kenani amemueleza Mgombea Urais Dkt. Samia kuwa wananchi hao wamekuja kwa wingi ndani ya viwanja vya leaders kutokana na kazi kubwa iliyowagusa maisha yao na kuacha alama chanya katika kipindi chake cha uongozi cha miaka 4 akiwa amekalia kiti cha Urais wa Nchi.
"..𝘞𝘢𝘯𝘢𝘯𝘤𝘩𝘪 𝘩𝘢𝘸𝘢 𝘸𝘢𝘮𝘦𝘬𝘶𝘫𝘢 𝘩𝘢𝘱𝘢 𝘬𝘸𝘢 𝘸𝘪𝘯𝘨𝘪 𝘬𝘶𝘵𝘰𝘬𝘢𝘯𝘢 𝘯𝘢 𝘬𝘢𝘻𝘪 𝘬𝘶𝘣𝘸𝘢 𝘶𝘭𝘪𝘺𝘰𝘪𝘧𝘢𝘯𝘺𝘢 𝘬𝘸𝘢 𝘬𝘪𝘱𝘪𝘯𝘥𝘪 𝘤𝘩𝘢 𝘮𝘪𝘢𝘬𝘢 𝘮𝘪𝘯𝘯𝘦 (4) , 𝘮𝘢𝘦𝘯𝘥𝘦𝘭𝘦𝘰 𝘦𝘯𝘥𝘦𝘭𝘦𝘷𝘶 𝘶𝘭𝘪𝘺𝘰𝘧𝘢𝘯𝘺𝘢 𝘺𝘢𝘮𝘦𝘨𝘶𝘴𝘢 𝘮𝘢𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘺𝘢𝘰 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘢𝘤𝘩𝘢 𝘢𝘭𝘢𝘮𝘢 𝘺𝘢 𝘮𝘢𝘵𝘰𝘬𝘦𝘰 𝘤𝘩𝘢𝘯𝘺𝘢 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘰𝘯𝘨𝘦𝘻𝘢 𝘵𝘪𝘫𝘢 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘣𝘪𝘢𝘴𝘩𝘢𝘳𝘢 𝘻𝘢𝘰, 𝘩𝘶𝘥𝘶𝘮𝘢 𝘻𝘢 𝘬𝘪𝘫𝘢𝘮𝘪𝘪 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘧𝘶𝘯𝘨𝘶𝘢 𝘶𝘬𝘶𝘢𝘫𝘪 𝘸𝘢 𝘶𝘤𝘩𝘶𝘮𝘪 𝘸𝘢 𝘮𝘵𝘶 𝘮𝘮𝘰𝘫𝘢 𝘮𝘮𝘰𝘫𝘢"
Huu ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM na sasa ni zamu ya Wilaya za Kinondoni na Ubungo Jijini Dar es salaam.
</

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇