Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuongeza boti za uvuvi za mikopo kwa wavuvi katika Ziwa Victoria wilayani Muleba ili kuongeza fursa zaidi kwa wavuvi.
"Vile vile tutaangalia uwezekano wa kuongeza boti za kisasa kwa wavuvi ili waweze kukua zaidi,"amesema Dkt. Samia.
Aidha, DKT. Samia amesema kuwa wanapoenda Mbele wakipewa ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kumpigia kura!katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, katika mkakati wao wa kuanzisha na kuendeleza kongani za viwanda, watangalia pia suala la usindikaji wa mazao ya uvuvi ili wavuvi wapate manufaa zaidi.
Dkt. Samia ametoa ahadi hizo na nyinginezo alipokuwa akijinadi yeye, wagombea ubunge na madiwani wa Chama hicho katika mkutano wa Kampeni za CCM wilayani Muleba mkoani Kagera Oktoba 15, 2025.
Pia, Dkt. Samia amesema kuwa Serikali anayoiongoza imetoa zaidi ya sh. Bil. 3 kwa ajili ya kujenga Soko kubwa la Kisasa la mazao ya uvuvi wilayani humo.




No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇