Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Mhe. Richard Msongwa, Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya
Malawi na Mkuu wa Misheni ya
Jumuiya ya Maendeleo Kusini
Mwa Afrika (SADC).
Mazungumzo yao yamehusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Jopo la Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) lipo nchini kufuatilia hatua za maandalizi ya uchaguzi huu wa saba tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ikiwa ni kielelezo cha uimara wa demokrasia nchini. 🇹🇿🗳️






No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇