LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 11, 2025

WENGI WAAPUZIA MAANDAMANO, WATAPIGA KURA OKTOBA 29

 



𝘼𝙨𝙚𝙢𝙖 𝙬𝙖𝙢𝙚𝙖𝙢𝙪𝙖 𝙠𝙪𝙟𝙞𝙚𝙡𝙚𝙠𝙚𝙯𝙖 𝙠𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚 𝙠𝙪𝙘𝙝𝙖𝙥𝙖 𝙠𝙖𝙯𝙞 𝙣𝙖 𝙠𝙪𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙖 𝙢𝙖𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙤 𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙫𝙪 𝙠𝙪𝙥𝙞𝙩𝙞𝙖 𝙢𝙜𝙤𝙢𝙗𝙚𝙖 𝙐𝙧𝙖𝙞𝙨 𝘿𝙠𝙩. 𝙎𝘼𝙈𝙄𝘼.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Ndugu. Paul Makonda, amemueleza Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 kuwa wananchi katika vijiwe mbalimbali alivyovitembelea wamemuhakikishia kuwa tarehe 29 Oktoba 2025 haitakuwa siku ya maandamano, bali siku ya kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura na wataendelea kuendeleza imani yao kwa chama hicho kwa kumchagua Dkt. Samia katika nafasi ya Urais, Wabunge na Madiwani wote wanaotokana na CCM.


Ndg. Makonda amebainisha hIlo mbele ya kadamnasi ya wananchi wa Shinyanga katika muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM, leo tarehe 11 Oktoba 2025.


Akieleza imani ya makundi mbalimbali ya watu aliyokutana nayo wakiwemo vijana wa bodaboda, wazee, akina mama lishe na wakulima kwa wafugaji, Ndg. Makonda amesema wananchi wamemueleza kwa dhati kuwa hawana nia ya kushiriki maandamano na kwamba wameamua kutumia haki yao ya kikatiba kwa kupiga kura na kuendelea kudumisha amani ya Taifa letu.


"..Wananchi hawana muda na mjadala wa maandamano, ni vema zaidi kuachana na mjadala huo na kuelekeza nguvu katika ushiriki wa uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia."


Aidha, Ndg. Makonda amewaeleza Watanzania dhamira ya dhati ya Dkt. Samia katika utekelezaji wa Ujenzi na Uboreshaji wa bandari mbalimbali nchini ambao umeongeza tija ya ukuaji wa kiuchumi na mwingiliano wa biashara wenye kuleta matokeo chanya katika kukuza na kuinua uchumi wa Watanzania na Taifa kwa ujumla kwa kusema kuwa Dkt. Samia amesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama zilizokuwa zikitumika awali na kuifungulia Tanzania milango ya uingizaji fedha nyingi kupitia bandari zetu fedha ambazo zimekuwa zikitumika pia katika utekekezaji wa miradi mingine ya kimkakati na kijamii.


Katika kumtakia Afya njema Mgombea Urais Dkt. Samia, Ndg. Makonda ametumia nafasi hiyo kumtakia afya njema na kumuombea Mungu huku akimsihi aendelee kufanya maamuzi yenye kuzingatia maslahi mapana ya Taifa la Tanzania kama afanyavyo sasa.


𝙐𝙨𝙞𝙗𝙖𝙗𝙖𝙞𝙨𝙝𝙬𝙚 𝙣𝙖 𝙫𝙞𝙟𝙞𝙢𝙖𝙣𝙚𝙣𝙤 𝙫𝙮𝙖 𝙪𝙤𝙣𝙜𝙤 𝙢𝙞𝙩𝙖𝙣𝙙𝙖𝙤𝙣𝙞, 𝙎𝙝𝙞𝙧𝙞𝙠𝙞 𝙪𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙯𝙞, 𝙢𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙚 𝘿𝙠𝙩. 𝙎𝘼𝙈𝙄𝘼 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙖𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙤 𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙫𝙪 𝙣𝙖 𝙠𝙪𝙞𝙣𝙪𝙖 𝙐𝙩𝙪 𝙬𝙖 𝙠𝙞𝙡𝙖 𝙈𝙩𝙖𝙣𝙯𝙖𝙣𝙞𝙖💚💛


#SafariYaCCM

#KaziNaUtuTunasongaMbele

#Oktoba29Tunatiki🇹🇿✅l

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages