LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2025

DKT. SAMIA AWAAHIDI MAKUBWA RUVUMA


MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kujenga barabara ya mchepuko kupunguza msongamano katika MJi wa Songea.

‎
‎Ametoa ahadi hiyo katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye viwanja vya Veta Msamala, Songea, akijibu ombi la Mgombea ubunge wa Jimbo la Songea MJINI, Dkt. Damas Ndumbaro Septemba 22, 2025.
 
‎
‎Amesema kuwa ombi hilo watalifanyia kazi kwa kujenga barabara ya mchepuko kuondoa foleni katika Mji huo.
 
‎
‎Rais, Dk.Samia amesema pia anatambua bado wananchi wana kiu ya barabara na madaraja. “Kipaumbele chetu tutakapoendelea ni kukamilisha miradi tuliyoianza alafu ndiyo tutashika ile mingine ambayo tumeianisha kwenye ilani ya uchaguzi.”
 
‎
‎Kuhusu mawasiliano ya simu amesema kuna maeneo ya Mkoa wa Ruvuma ambayo mawasiliano ya simu siyo mazuri. Hivyo nalo Serikali itakwenda kulifanyiakazi kuhakikisha mawasiliano ya simu yanakuwa mazuri kwa sababu ukanda wa biashara lazima uwe na urahisi wa mawasiliano," alibainisha.
 
‎
‎Pamoja na hayo amewaeleza wananchi hao wakati yeye akiendelea kuomba ridhaa ya kuomba kuendelea kuwatumia kuna watu wengine (wagombea) wanazunguka kama yeye ambao wananadi ilani zao.
 
‎
‎“Lakini kila nikiwasikiliza ni yaleyale yaliyopo kwenye ilani ya chama chetu lakini ndani ya ilani ya chama cha mapinduzi tukiandika tunajua tutatekeleza kwa njia gani. Fedha itatoka wapi, vipi tutakamilisha tuliyoyaandika suala siyo kusema tutafanya lakini vipi tutafanya hilo ndilo suala muhimu.
 
‎
‎“CCM tunasimama kujiamini na ujasiri mkubwa kuomba kura mtuchague tuendelee kuongoza serikali hii kwa sababu tumefanya mmeona na ninaamini tutaweza kufanya na mtaona.”
 
‎
‎Katika hatua nyingine Dk.Samia ameendelea kuwahamasisha wananchi ikifika siku ya kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu waende kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni yeye, wabunge na madiwani wa Chama hicho ili kasi ya kuleta maendeleo ya watanzania iendelee.
‎

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages