Tayari Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi. Dkt. Asharose Migiro amewasili na kupokelewa Viongozi mbalimbali wa Chama na Kidini pamoja na maelfu ya wananchi wa Kibaha mkoani Pwani katika viwanja vya sabasaba kwa Mbonde, wakiwa tayari kwa kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 anayetarajiwa kunadi sera na ahadi za CCM pamoja na kuomba kura za Ndiyo kwa mafiga yote matatu (Rais, Wabunge na Madiwani) leo tarehe 28 Septemba 2025.
Pamoja na hayo, wananchi wa Kibaha wametuma salamu zao za upendo kwa Rais Dkt. Samia ambazo wamemuomba Katibu Mkuu Dkt. Migiro kuziwasilisha kwake.
Huu ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM na sasa ni zamu ya mkoa wa Pwani.





No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇