CCM Blog, Kawe.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya Itikadi na Uenezi Kenani Kihongosi, ametoa mwito kwa wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za CCM, utakaorindima kesho katika viwanja vya Tangayika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.
Mwito huo ameutoa leo, wakati
kizungumza leo, Agosti 27, 2025, katika Viwanja hivyo, baada ya kukagua maandalizi ya uzinduzi huo.
Amesema CCM imejipanga kufanya kampeni za kistaarabu bila kutweza utu wa mtu na kusema wagombea walioteuliwa na Chama wamebeba matarajio makubwa ya wananchi, na kupitia kampeni hizo watapata nafasi ya kuwaeleza Watanzania yale yaliyotekelezwa na chama na pia mipango iliyopo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
“Wagombea waliochaguliwa na Chama Cha Mapinduzi wanasifa zote za kuwa viongozi. CV zao zimejitosheleza, na pia wamebeba matumaini makubwa ya wananchi wa Tanzania,” alisema.
Kihongosi aliongeza kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM imebeba mambo makubwa na matumaini, huku ikitoa majibu kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Aliwaomba na kuvialika vyama vingine vya siasa kufika katika uzinduzi huo ili kusikiliza sera na Ilani ya CCM, akisisitiza kuwa chama hicho kitatumia jukwaa hilo kueleza sera zake na kuwanadi wagombea wake wa Kata na majimbo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇