LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 29, 2025

DKT. DIMWA AKAGUA MAANDALIZI YA KUHITIMISHA UCHUKUAJI FOMU ZANZIBAR


Na Dismas Lyassa, Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohammed Said Mohammed Dimwa, leo amefanya ukaguzi wa eneo la viwanja vya Mau tse Tung, ambalo kesho Jumamosi, tarehe 30 Agosti 2025, Chama Cha Mapinduzi kinatarajia kutumia kuhitimisha shughuli ya kihistoria za uchukuaji wa fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar.


Akiwa katika eneo hilo, Dkt. Dimwa ameeleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa na kueleza kuwa maandalizi yamefikia ukingoni, huku kila kitu kikiwa tayari kwa tukio hilo muhimu.


Shughuli ya kesho itaongozwa na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiambatana na viongozi wakuu wa CCM na jumuiya zake, huku viongozi wa dini wakitarajiwa kutoa baraka na maombi ya kuliombea Taifa amani na mshikamano.


Maandalizi ya kesho yanatarajiwa kuhakikisha tukio hili linafanikiwa kwa heshima na nidhamu, huku CCM ikijiweka tayari kuendeleza mshikamano na maendeleo ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages