LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 15, 2025

WANANCHI MANYONI WAMTAKA SULTAN NASSOR: WAFANYA DUA NA SALA KUMUOMBEA UBUNGE


Na Mwandishi Wetu, Manyoni

Wananchi wa Jimbo la Manyoni wamejitokeza kwa wingi na kwa shauku kubwa wakimtaka Kada maarufu wa CCM, Sultan Nassor Sultan ([pichani), kuwa mgombea wao wa ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakieleza kwa mshikamano kuwa ndiye kiongozi wanayemhitaji kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Wengine wamekuwa wakifanya dua na sala maalum wakimuombea Sultan mafanikio katika safari yake ya kisiasa, wakimtaja kuwa ni mkombozi wa wanyonge na mtu wa vitendo, si maneno.

Sultan Nassor Sultan, ambaye tayari amechukua na kuirudisha rasmi fomu ya kugombea ubunge, ni jina linalobeba matumaini kwa wakazi wa Manyoni kutokana na kazi nyingi alizozifanya ambazo zimegusa maisha ya watu wa makundi mbalimbali.

Kiongozi wa Watu, Mshirika wa Maendeleo

Sultan amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana kwenye michezo kwa kuwapatia jezi, mipira na vifaa vingine mara kwa mara. Kwa sasa, amewakabidhi vijana jezi mpya kwa ajili ya kushiriki Ligi ya Mwenge, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuwajenga vijana kimaadili na kuwapa matumaini kupitia michezo.

Mchango kwa Sekta ya Elimu

Katika sekta ya elimu, Sultan amekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wasiojiweza kwa kuwapatia madaftari, kalamu, zawadi mbalimbali na chaki kwa shule. Katika Shule ya Msingi Kamenyanga (jina linahakikiwa), Sultan alitoa boksi kadhaa za madaftari, kalamu, mipira miwili na boksi la chaki ili kusaidia mazingira ya kujifunzia.

Kumhudumia Mwananchi wa Kawaida

Sultan pia amekuwa akisaidia vifaa vya ajili kwa ajili ya majengo ya chama, na yale ya kijamii, kwa mfano miezi kadhaa nyuma alitoa tofali 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT kama ishara ya mshikamano wa kidini na kijamii, huku akihakikisha kuwa kila mchango wake unalenga kuweka alama ya upendo, umoja na maendeleo.

Zaidi ya hayo, amechimba visima viwili vya kina virefu katika eneo la Manyoni Chang’ombe, ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo yenye shida ya maji. Visima hivyo vinatoa huduma ya maji bure kwa wananchi.

Ajira na Uchumi wa Ndani

Kupitia kiwanda chake cha mikate, Sultan ameweza kuajiri vijana wengi katika maeneo ya uzalishaji, uuzaji na usambazaji. Aidha, maduka yanayomilikiwa na kuendeshwa na vijana chini ya mpango wake wa ujasiriamali, yameongeza fursa za kipato kwa wananchi wa kawaida.

Wakazi wa Manyoni wamesisitiza kuwa Sultan ni chaguo la wananchi, mwenye rekodi ya uwajibikaji na moyo wa kujitoa, na kwamba sasa ni wakati wa kumpa nafasi ya kuwatumikia kwa ngazi ya juu zaidi.

“Ameshafanya mengi bila kuwa mbunge. Akipewa ridhaa, tuna uhakika atasimamia haki zetu na kuleta maendeleo kwa kasi zaidi,” alisema Mama Juliana Hambwe, mkazi wa eneo la Kinyamwezi.

Sultan mwenyewe alipotafutwa kuulizwa kama anajua chochote kuhusiana na taarifa za wananchi kufanya sala na dua kwa ajili yake, alisema hana taarifa hizo na akawaomba wana Manyoni kuendelea kuwa na utulivu wakati huu ambao chama kinaendelea na mchakato wa kuteua wagombea.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages