LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 31, 2025

DEVOTHA, SAMILA KIDEDEA UBUNGE VITI MAALUM UWT KAGERA

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Wanachama wa Jumuia ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Devota Daniel Mburarugaba na Samila Khalfan Amour wamejipatia ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Wabunge Viti Maalum mkoa wa Kagera, uliofanyika jana.


Katika matokeo yaliyotangazwa baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuia hiyo, Devota aliongoza kwa kupata kura 1,308, akifuatiwa na Samila aliyepata kura 1,250. Ushindi wao umetangazwa rasmi, na sasa watawakilisha Mkoa wa Kagera katika Bunge.


Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Devota aliwashukuru wajumbe kwa imani yao, akiahidi kufanya kazi kwa karibu nao katika kuimarisha chama na kuhakikisha wanakusanya kura nyingi za urais kwa Dk. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwezi Oktoba.


Kwa upande wake, Samila alieleza kuwa ushindi huu ni alama ya umoja wa wanawake wa Kagera, akiahidi kuifanya kazi kwa juhudi kubwa ili kuimarisha chama na kuleta maendeleo katika mkoa huo.


Kulingana na Katibu wa UWT Mkoa wa Kagera, Rehema Zuberi, jumla ya wajumbe 1,556 walihudhuria na kupiga kura katika uchaguzi huo, ambao ulisimamiwa na wasimamizi wawili na kuridhiwa na Kamati Kuu ya UWT Taifa. 


Ushindi huu wa wanawake wawili kutoka Kagera unatoa taswira nzuri ya ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wanawake katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kisiasa.

Devota Daniel Mburarugaba na Samila Khalfan Amour.
Devota Daniel Mburarugaba na Samila Khalfan Amour wakiwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni.
Wajumbe.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages