Jun 6, 2025

RAIS DK. SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA RAIS MSTAAFU WA ZAMBIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ametuma salam za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Zambia Edga Chagwa Lungu.


“Nimesikitishwa sana kusikia taarifa za kifo cha Rais wa zamani wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu.

Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu za rambirambi za dhati kwa Mheshimiwa Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia, familia ya Rais Lungu, marafiki na wananchi wote wa Zambia", amesema Rais Dk. Samia kwente mtandao wa Instagram.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages