Jun 1, 2025

GAVANA BWANKU AINGIA VITONGOJINI NA WATENDAJI, POLISI KATA KUMALIZA MIGOGORO YA WANANCHI PAPO KWA PAPO

Katerero inafurahia mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan huku migogoro ya hapa na pale ya wananchi ikiendelea kutupwa kule.


Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku amejitengenezea ratiba ya kuhakikisha siku 3 ndani ya wiki anatatua migogoro ya wananchi na kufanya ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Tarafa na wiki hii ilikua zamu ya Kata ya Katoro.


Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera, Bwanku M ameongozana na Mtendaji wa Kata ya Katoro, Hamza Masudi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Katoro Yahya Azizi na Mtendaji wake Devis Shubi pamoja na Polisi Kata Afande Sylivester Maige pamoja na Wenyeviti wa Vitongoji kutatua migogoro ya wananchi kwenye Vitongoji.


Ndani ya utatuzi huo wa migogoro, mambo mengine mtambuka ndani ya jamii yamekua yakisisitizwa na kuelezwa ikiwemo wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo kudumisha ulinzi na usalama, kusisitiza wananchi kuishi kwa upendo na kupunguza migogoro, mafanikio makubwa ya maendeleo yanayofanywa na Serikali ya Rais Samia n.k

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages