Ilemela, Mwanza
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ameongoza mamia ya waombolezaji, katika kuaga mwilitoaji na maziko ya Mzee Silvin Ibengwe Emmanuel Mongella, katika Kijiji cha Kabusungu, Ilemela, mkoani Mwanza, jana, Juni 7, 2025.
Mzee Mongela ni Baba wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM John Mongella na pia aliyekuwa mume wa mmoja wa viongozi waandamizi wastaafu nchini, Getrude Mongella,
Shughuli hiyo ya mazishi ya Mzee Mongella, ilitanguliwa na ibada ya misa takatifu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, ikiongozwa na Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, huku mahubiri yakitolewa na Padri George Nzungu.
Viongozi wengine waliojumuika pamoja na waombolezaji katika mazishi hayo ni pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Jumuiya ya Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, mawaziri, viongozi waandamizi wa Chama na Serikali, wabunge na viongozi wa kiroho kutoka madhehebu ya dini mbalimbali nchini.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akimpa pole Mama Getrude Mongella. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM John Mongella.Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi akimpa polea John Mongella.Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza katika msiba huo.Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye msiba huo.
Waombolizaji katika msiba huo.
Mama Mongella akiweka mchanga kaburini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇