Jun 1, 2025

ALHAJI SONGAMBELE AMBAYE NI MIONGONI MWA WAANZILISHI 30 WA TANU AMEFARIKI DUNIA

Dar es Salaam
Mwanasiasa mkongwe ámbaye ni miongoni mwa wapigania Uhuru wa Tanganyika, Alhaj Mustafa Mohamed Songambele, amefariki dunia jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na binti yake Dorah Songambele, ambaye amesema maandalizi ya kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda Songea kwa ajili ya  maziko yanaendelea na msiba upo nyumbani kwake Mwananyamala.

Marehemu Songambele alitimiza umri wa miaka 100 Jumapili iliyopita Mei 25, 2025, na kusherehekewa na familia na marafiki wa karibu. 

Alhaj Songambele  alikuwa mmoja wa waanzilishi 30 wa TANU, na baadaye CCM, akiwa na kadi namba 27. 

Aliweka rekodi ya kuwa  Mkuu wa Wilaya wa kwanza nchini, alipoteuliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
kuongoza  Wilaya ya Pwani (sasa Ilala) na baadaye kupandishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
 
Mzee Songambele pia anatajwa kuwa miongoni mwa wana Dar es salaam waliompokea Mwalimu Nyerere alipoacha kazi ya ualimu na kuongoza harakati za uhuru, na ndiye aliyemsaidia kupata kiwanja cha kujenga nyumba yake eneo Magomeni Mikumi, nyumba ambayo sasa ni makumbusho ya Baba wa Taifa.

Marehemu Alhaj Mustafa Mohamed Songambele

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages