May 19, 2025

PURA YATOA UTEKELEZAJI NA MAFANIKIO KIPINDI CHA SERIKALI YA AWAMU YA SITA CHINI YA RAIS DK. SAMIA. YAJAZA GESI FUTI BILIONI 301.33 MIAKA MINNE

Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Charles Sangweni, akizungumza katika kikaokazi baina ya PURA na Wahariri na Waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam, leo Mei 19, 2025.

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Dar es Salaam
Kufuatia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuchukua hatua ya kuhakikisha Wananchi wanatambua kwa kina inavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2020-25, kupitia Mashirika na Taasisi zake za umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina imekuwa ikiratibu Mikutano baina ya Wahariri na Mashirika na Taasisi za Umma, ili kuwajengea Wahariri hao ufahamu wa majukumu na utekelezaji wa kazi zinazofanywa na Mashirika na Taasisi husika.

Katika mwendelezo wa hatua hiyo, leo Mei 19, 2025, ilikuwa zamu ya Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), ambapo ilifanya kikao kazi jijini Dar es Salaam na Wahariri na Waandishi wa habari, na kutoa tarifa ya Utekelezaji wa Majukumu na Mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongzwa na Rais Dk. Samia.

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka hiyo (PURA), Charles Sangweni amesema, kwa kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Machi 2025 kiasi cha gesi kilichozalishwa kimefikia futi za ujazo bilioni 301.33 na kwamba kipindi cha nyuma uzalishaji wa nyuma ulikuwa wastani wa futi za ujazo bilioni 32.03 kwa mwaka kwa upande wa Mnazi Bay na futi za ujazo bilioni 25.13 kwa mwaka upande wa Songosongo.

Amesema gesi hiyo ilianzishwa ili itumike  kwa matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwandani, majumbani, taasisi na katika magari.

Katika Kikao hicho Wahariri walipata fursa na kuuliza maswali au kutoa ushauri baada ya taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa PURA
TAARIFA KAMILI HII HAPA.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages