May 25, 2025

MWENYEKITI MTAA WA MBEZI BEACH ‘A’ AFANYA KIKAO NA WANANCHI KUELEZA MIKAKATI NA MAENDELEO YA MTAA HUO KWA KIPINDI KILICHOISHIA APRILI 30, AELEZA HALI YA UJENZI WA OFISI YA MTAA




Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Beach A Esther Mwamyalla akizungumza katika kikao chake na Wananchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rainbow, Mbezi Beach, Kawe Jijini dar es Salaam, jana, Mei 24, 2025.

Wananchi na Wakimsikiliza Mwenyekiti Mwamyalla katika kikao hicho.
Mwenyekiti Mwamyalla, akifafanua mambo mbalimbali na kuwashukuru wananchi kwa kuhudhuria kwa wingi, kabla ya kufunga kikao hicho.

Na Bashir Nkoromo, Mbezi Beach A
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Beach A, Kata ya Kawe Wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Esther Mwamyalla jana, Mei 24, 2025 alifanya Kikao na Wananchi wa mtaa huo, ambacho alikitumia kutoa Taarifa ya Maendeleo ya Mtaa huo katika huduma mbalimbali kwa kipindi kilichoishia Aprili 30, mwaka huu.

Pamoja na mambo mengine, Mwenyekiti Mwamyalla alieleza maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa huo, ambayo wakati uongozi uliopo madarakani ulipoingia ulikabidhiwa jengo la ofisi hiyo ujenzi wake ukiwa umeishia kwenye 'linta' na kwamba ili kupata fedha za kuendeleza ujenzi huo, viongozi wa sasa waliona ni vyema kufanya changizo (harambee) kwa ajili ya kupata fedha za kuukamilisha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tarehe 01/02/2025 Mwenyekiti Mwamyalla, alimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  kuendesha chagizo la ujenzi wa ofisi hiyo na kueleza kwamba katika harakati za kuhamasisha changizo hilo. 

Mwenyekiti Mwamyalla akasema, katika harakati za kuhamasishana ni  wakazi 37 walikamilisha ahadi zao 31 bado hawajakamilisha ahadi zao akifafanua kwa wakazi wengi hawajalipa au kutoa ahadi wakisubiri mgawanyo wa mchango wa bajeti ya ujenzi kama waliivyokubaliana kwenye kikao.

Akiendelea kutoa taarifa hiyo, Mwenyekiti Mwamyala alieleza mpango wa maendeleo katika kipindi kilichishia Aprili 2024, ambapo alisema utekelezaji wa mpango huo ni muendelezo wa mipango iliyopangwa awamu iliyopita na kwamba imegawanyika katika sehemu kuu sita (6) zinazo kusimamiwa na kamati. Kamati hizo ni  Ulinzi na Usalama,  Miundo Mbinu,  Mazingira, Jamii,  Michezo na Elimu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages