May 2, 2025

MKURUGENZI MTENDAJI MEATU, ZAHARA MICHUZI ANYAKUA TUZO YA MFANYAKAZI HODARI, MEI MOSI 2025

Na Mwandishi Maalum
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Zahara Muhidin Michuzi jana, aliibuka na siku njema, kufuatia kututunukiwa tuzo ya Cheti kuonyesha kutambuliwa mchango wake mkubwa kama mfanyakazi hodari na mwenye weledi, katika sherehe zaa Maadhimisho ya Mei Mosi zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa  Nyuzo Nane Wilayani Maswa.

Tuzo hiyo imetolewa kama sehemu ya kuthamini juhudi za viongozi na watendaji wanaoonyesha juhudi, kujituma, uzalendo wa kweli, ufanisi na uongozi thabiti katika utumishi wa umma, hasa katika, kusimamia miradi maendeleo, ukusanyaji wa mapato, kutatua kero za watumishi na wananchi kwa ujumla sanjari na kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza baada ya kumkabidhi tuzo hiyo, RC Kihongosi aliwasihi watumishi wa umma mkoani Simiyu kuiga mfano wa Zahara kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha alama nzuri zisizofutika, uwajibikaji na moyo wa kizalendo.

Zahara alihamishiwa Wilayani Meatu mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu, akitokea Wilaya ya Kilombero, Halmashauri ya Mji Ifakara mkoani Morogoro, ambako pia alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji huo.

Kabla ya hapo, Zahara alikuwa Mkurugenzi wa Mji Geita katika Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita akifanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotambuliwa na wengi na kuacha alama zisizosahailika.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi, alikabidhi cheti cha heshima kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Bi. Zahara Muhidin Michuzi kwa kutambua mchango wake mkubwa kama mfanyakazi hodari na mwenye weledi, cheti hicho alikabidhiwa katika shamrashamra za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, katika Uwanja wa Nguzo Nane Wilayani Maswa.
Zahara akipongezwa.
Cheti cha kutambuliwa.
Zahara akiwa na wezake kwa mshikamano.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages