May 30, 2025

MATUKIO YA UZINDUZI WA ILANI MPYA YA CCM 2025 - 2030

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2025-2030 kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara Ndugu Stephen Wasira mara baada ya kuizindua kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 30 Mei,2025.

Dkt. Samia akiwa na Makamu Mweenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Visiwani, Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiwa na vitabu vya Ilani baada ya kuzinduliwa.


Dkt. Samia akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2025-2030 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 30 Mei,2025.


Dkt. Samia akihutubia katika mkutano huo.






No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages