Apr 23, 2025

POLISI: WANAFUNZI TOENI TAARIFA WENZENU WAKICHEZA NA KUZURURA MITAANI WANAPOTOKA SHULE

Na Issa Mwadangala, Songwe
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limewapa mbinu wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoani hapa, kutoa taarifa za wanafunzi wenzao ambao wamekuwa wakizurura na kucheza mitaani pindi watokapo shuleni ili waepukane na kufanyiwa vitendo vya ukatili wanavyoweza kukumbana navyo njiani.

Kauli hiyo ilitolewa Aprili 22, 2025 na Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicholas Livingstone ambapo amesema kitendo cha wanafunzi kucheza mtaani pindi watokapo shule kinaweza kuwapelekea kufanyiwa vitendo vya ukatili kitendo na unyanyasaji dhidi yao ambacho kitawarudisha nyuma kimasomo na kushindwa kutimiza malengo ya masomo na maisha yao ya baadae.

Aidha, ACP Livingstone amewataka wanafunzi hao wanapowaona wenzao wanacheza na kuzurura mtaani pindi watokapo shuleni watoe taarifa kwa walimu au wazazi wao ili waweze kutatua tatizo hilo kwa haraka.

Pamoja na mambo mengine, ACP Livingistone amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza na kuwatii wazazi na walimu ili waendelee kuwa na maadili mema katika jamii.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages