Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deodatus Mwanyika amesema kuwa kuja haja kubwa ya serikali kuzitambua mbegu za asili kwani zina umuhimu mkubwa ama sivyo zitapotea kabisa.
Pamoja na mambo mengine ameyasema hayo wakati kamati hiyo ilipokutana na kikosi kazi cha wakulima bungeni Dodoma Aprili 18, 2025, kinacholitaka Bunge litunge sheria ya kuzitambua mbegu hizo za asili
Mwanyika (wa pili kulia) na Mama Salma Kikwete wakiwa na wabunge wengine wakinunua mbegu za asili za mazao mbalimbali baada kumalizika kwa kikao chao.
Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa kikao hicho na kusisitiza kuundwa haraka kwa sheria ya kuzitambua mbegu hizo za asili.
Mbunge wa Viti Maalumu, Shally Raymond akichangia mada katika kikao hicho.
Baadhi ya wakulima wa kikosi kazi hicho wakiongozwa na Daudi Manongi (pichani) ambao wamefanya utafiti juu ya umuhimu wa mbegu hizo wakiiomba kamati hiyo kuhimiza uundwaji wa sheria ya kuzitambua mbegu hizo.
Baadhi ya wabunge wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika kikao hicho.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇