Makamu Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewahakikishia wananchi wa Tunduma na mkoa wa Songwe kwa ujumla kuwa serikali ina fhamira ya dhati kutatua changmoto zao hususan ya maji na upanuzi wa barabara.
Wasira ameeleza hayo leo Machi 15, 2025 alipokuwa akiwahutubia wananchi mjini Tunduma, wilayani Momba Mkoa wa Songwe ambapo amesema kwa upande wa kero ya msongamano wa malori katika mji huo ufumbuzi utatokana na kupanuliwa kwa barabara ya Mbeya-Tunduma kuwa ya njia nne.
Amesema atakutana na Waziri wa Miundombinu (Abdallah Ulega) na atamfikishia ombi la wananchi wa mkoa huo kutaka upanuzi wa barabara hiyo ambao tayari umeanza mkoani Mbeya uwe na wakandarasi wawili ambapo mwingine aanzie Tunduma kuelekea Mbeya na hatimaye wakutane katikati kwa lengo la kuongeza kasi ya ujenzi.
==
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tunduma akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Songwe.(PICHA NA Fahadi Siraji)Wananchi Wakishangilia katika mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira uliofanyika mjini Tunduma akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Songwe.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, leo Machi 15, 2025, akishiriki ujenzi wa Shule ya Sekondari Ukwile alipoitembelea akiwa katika ziara mkoani Songwe.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, akipata maelezo kuhusu Hospitali ya Mkoa wa Songwe alipoitembelea akiwa katika ziara mkoani humo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, leo Machi 15, 2025 alipotembelea Shule ya Msingi Hiloli iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe na kupata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo wanaojiandaa na mtihani wa taifa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇