Dkt Dismas Lyassa na Vikta Makinda, Shinyanga
Meya ya Manispaa ya Shinyanga Mjini, ndugu Elias Masumbuko (pichani) amempongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mzuri wa Ilani katika kipindi chake cha miaka minne madarakani kama Rais wa Tanzania.
“Manispaa ya Shinyanga tumenufaika pakubwa sana kutokana na jitihada za mheshimiwa Rais Samia, kwa mfano katika Kata ya Chamagoha ambako mimi ni Diwani wake, tumekuwa hatuna daraja, lakini Rais Samia alituletea milioni 470 ambazo zimetumika kujenga daraja jipya na zuri linalounganisha kata ya Changagoha na Kata ya Kitangili,” anasema meya huyo.
Amefafanua kuwa karibu kila sekta zimeguswa zikiwamo elimu, miundombinu, afya, maji, na huduma za kijamii.
Meya huyo ameeleza mafanikio makubwa kwenye sekta ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli na uboreshaji wa barabara na madaraja yaliyo korofi kama vile la Uzogole, Iwelyangula, na Kitangili.
Amesema pia kuwa Rais pia ameboresha miundombinu ya afya, ikiwa ni pamoja na kituo cha afya cha Kambarage, hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na Hospitali ya Rufaa.
“Hakika Rais Samia ametuheshimiwa sana na tuendelee kumuunga mkono,” anasema Meya Masumbuko.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇