Na Lydia Lugakila, Kagera
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeweka kipaumbele katika kutatua changamoto za vijana, hasa suala la ajira kupitia Ilani yake ya Uchaguzi mkuu wa 2025-2030.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM Tanzania Bara, Stephen Masato Wasira, machi 22, 2025, akiwa Mkoani Kagera alipohutubia Wananchi wa kata ya Kemondo, Wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera, katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuimarisha uhai wa chama sambamba na kutatua kero mbali mbali zinazowakabili Wananchi Mkoani humo.
“Chama cha Mapinduzi kinaelewa bayana changamoto za vijana na mara kwa mara kimekuwa na mikakati imara ya kuzitatua changamoto hizo" Wasira.
Mhe, Wasira amesema kuwa katika kumbukumbu chama kiliasisiwa na vijana katika kipindi ambacho Mwalimu Nyerere alikuwa na miaka 32.
Ameongeza kuwa chama hicho hakiwezi kuwa chama cha wazee pekee, bali kitahakikisha vijana wanapata nafasi na suluhisho la changamoto zao ili wakifurahie chama hicho na kuitumikia vyema nchi yao" alisema Wasira.
Aidha amesisitiza kuwa Ilani ijayo ya Chama cha mapinduzi itaweka msukumo maalum kwa maendeleo ya vijana, ikiwemo fursa za ajira na ushiriki ili kila kijana apate kunufaika vyema na matunda ya Nchi yake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇