Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza matembezi ya hisani ya Kilomita tano (05) kuadhimisha miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yatakayofanyika Machi 7, 2025.
TET imesema, kaulimbiu ya matembezi hayo ni 'Kitabu Kimoja Mwanafunzi Mmoja' na yataanzia eneo la Utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Chuo cha Maji, Mlimani City, Mwenge na kuishia ofisi za TET makao makuu.
imewakaribisha wananchi wote kujisajili kwenye matembezi hayo ili kuwa sehemu ya maboresho ya elimu nchini kwa kuchangia upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari.
"Karibu ujisajili kwenye matembezi ya hisani ya Kilomita tano (05) kuadhimisha miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Jisajili sasa kwa TZS 50,000/= upate tisheti au TZS 150,000 upate track suit.
Scan QR CODE kujisajili au tumia link Bofya Hapa", imesemaTET.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇