Ni mwisho wa Mbowe au mwanzo wake?
Toka Mbowe akumbwe na mapinduzi "coup d'etat" hajaonekana akijihusisha na shughuli yoyote ya chama ambacho aliahidi mara kadhaa "kukilinda kwa wivu mkubwa" na kudai amepata hasara kubwa kukijenga.
Hata kukabidhi ofisi hakuonekana!
Sasa mpaka mwanawe James amezuia vyombo vyake kutumika kwenye mkutano wa chadema.
Je huu ni mwisho wa Papaa? Is it the end of the beginning or the beginning of the end?
Kuna hasara ipi aliyeondoka ofisini kususa makabidhiano na kutojihusisha na taasisi ambayo aliapa atailinda kama mboni ya jicho lake?
Tayari tunamuona mrithi au aliyempindua akitwmbeza bakuli kiasi cha kuomba hata maji chupa!
Mrithi badala ya kueleza amejipangaje kwa uchaguzi mkuu kajikita kwenye misamiati aka semantics za 'no reform no election but no kususia"! Sasa kaongeza unashiriki "ili iweje"!
Na kutokana na hulka yake Lazima ataenda jela. Anadai "nchi iwake moto tuanze upya". Hiki ndio kitaharakisha safari yake kumfuata padre gesti ya serikali. Kukaa kwake jela kutadhoofisha mno CHADEMA version 2. Msaidizi wake yule mura ni mtu asiyetaka jela. Muda wote alijitahidi kuepuka kwenda jela. Yeye na kina John Mrema, Kibaila n.k. hawajawahi kudakwa.
Ukweli kila mtanzania anaujua. Uchaguzi utakuwepo bila reform ya katiba, tume Wala taratibu. Ni Mjinga tu anaamini kutakuwa na katiba, tume na utaratibu mpya between now and October!
Nionavyo itakuwa hivi: Lissu na timu yake watashindwa kugharamia uchaguzi mkuu. Watampata Mzee kugombea uraisi. Wataaamua kususa ama kushiriki wakiwa wamesimamisha chini ya asilimia 20 ya wagombea. Watashindwa vibaya kuliko 2020. Patazuka vuguvugu la BRING BACK MBOWE ambalo Lissu na kikosi chake watashindwa kulidhibiti. Ikifika February 2026 Mbowe atakuwa karudi tena CHADEMA. A new beginning !
Na utakuwa mwisho wa Lissu.
Don't say I didn't tell you
Imeandikwa na Sheikh Yahya Msangi au Mlamba Asali wa KImataifa.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇