LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2025

MBUNGE RWEIKIZA AWATAKA UVCCM WILAYA YA BUKOBA KUTAMBUA MAZURI YA RAIS DK. SAMIA

Na Lydia Lugakila, Bukoba.

Mbunge wa Bukoba vijijini Dokta Jasson Rweikiza amewataka vijana wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera kuwa  mstari wa mbele kukisemea Chama  hasa kutambua mazuri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan


Dokta Rweikiza ametoa kauli hiyo wakati akizungumza  na vijana wapatao 285 kutoka kata 29 za Wilaya ya Bukoba katika mafunzo maalum ya yaliyoandaliwa na UVCCM wilaya ya Bukoba yaliyolenga kuwajengea uwezo Wenyeviti, Makatibu wa umoja huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Bukoba Resort uliopo kata Kemondo Wilayani humo


"Mwaka huu ni wa uchaguzi lazima vijana mjitambue kukisemea chama ili kisonge mbele pia mtambue mazuri yaliyofanywa na Rais Samia hasa katika Wilaya yetu kwani tumejionea miradi mikubwa ikiwemo ya maji, umeme, Barabara, Hospitali, kujengwa kwa vituo vya afya, Madaraja makubwa" alisema Dokta Rweikiza.


Rweikiza amesema ni vijana hao wanatakiwa kuyasemea mazuri yaliyofanywa na viongozi wao ikiwa ni pamoja na kuisoma  ilani na katiba ya chama cha Mapinduzi ili waelewa malengo ya chama hicho pamoja na kanuni ya UVCCM ili waifahamu  na ikitokea wamekutana na watu wanaobeza chama wawajibu kwa hoja.


Mbunge huyo aliongeza kuwa Vijana hao pia wanatakiwa kuendelea kutunza amani na utulivu kwani Nchi nyingi bado zinataabika na migogoro inayosababisha machafuko.


Hata hivyo Mbunge huyo amewatahadharisha Vijana hao juu ya matumizi mabaya ya ki mtandao huku chama hicho kikisema hakitahusika kwa namna yoyote ile pale kijana atakayekiuka  sheria ya mtandao hata kama atakuwa ni kiongozi wa chama hicho.


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages