Mama Lishe wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Februari 4, 2025, tayari kuongoza maadhimisho ya miaka 48 ya CCM kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kesho.
CCM Itatumia maadhimisho hayo kuwatambulisha kwa wana CCM wagombea wao urais kupitia chama hicho katika uchaguzi Mkuu ujao. Samia atagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mgombea Mwenza atakuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi. Dkt. Hussein Ali Mwinyi atagombea urais wa Zanzibar.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇