LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 23, 2025

KATIBU KATA CCM HEKA MANYONI AMPONGEZA RAIS SAMIA

Na Dkt Dismas Lyassa, Manyoni


Katibu wa CCM Kata ya Heka, Jimbo la Manyoni Mashariki, ndugu Elisha Ndagwa amempongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusimamia vizuri nchi na chama kwa ujumla. Akizungumza na CCM Chama Blog, Katibu huyo anasema maendeleo katika kata yake yamekuwa ni makubwa na kwamba anawaomba Watanzania kumpa ushirikiano wa kumchagua tena ili aendeleze maendeleo nchini.

Kiongozi huyo anapongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Rais na Mwenyekiti huyo wa CCM ikiwamo kugawa pikipiki kwa makatibu kata wa CCM kitendo ambacho anasema ni mpango mzuri wa kuongeza ufanisi katika ngazi za chini.

Katibu wa CCM Kata ya Heka, ndugu Elisha Ndagwa. (Picha na Vikta Makinda)


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages