Na Dkt Dismas Lyassa, Manyoni
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Manyoni, ndugu Jumanne Ismail Makhanda amewaasa viongozi wenzake kuendelea kuwa wabunifu wa miradi ya kiuchumi ili kuongeza kipato ndani ya chama kama njia ya kukifanya chama hicho kuendelea kuwa na imara na kuwe na meno ya kuwawajibisha watumishi pale wanapoonekana kwenda kinyume na taratibu za kazi.
Akizungumza katika mahojiano ofisini kwake, mwenyekiti huyo anawaasa viongozi wa ngazi mbalimbali kubuni miradi inayoweza kuingiza kipato, kwani kwa kufanya hivi kutasaidia sana kuondokana na utegemezi wa wadau au viongozi wa Serikali.
”Ni jukumu letu sisi viongozi wa chama kuisimamia Serikali na wakati mwingine kuiwajibisha, lakini unawezaje kwa mfano kumuwajibisha mwenyekiti wa kijiji au mtaa, Diwani au Mbunge ikiwa shughuli zote za chama ndiye unayemtegemea hata kukodi viti vya mikutano au mafuta,” alisema mwenyekiti huyo.
Akasisitiza kwamba anashauri viongozi wa chama wa ngazi zote kuendelea kubuni njia mbalimbali za kujitegemea kiuchumi.
”Wakati naingia kwenye nafasi hii ya uenyekiti wa wilaya nilibuni mambo kadhaa, mojawapo ya kuhakikisha tunajenga fremu nyingi za biashara, pia kujenga ukumbi mkubwa kwa ajili ya shughuli za chama na pia kukodisha, naamini sisi viongozi wa chama tunaweza kufanya haya na zaidi ya haya ili kuhakikisha chama chetu kinakuwa imara kiuchumi. Imani yangu siku zote ni kwamba pale chama tunapokuwa imara kiuchumi, inakuwa rahisi kumuwajibisha kiongozi yeyote bila hofu, tofauti na vile ambavyo unayemuwajibisha ndiye unayemtegemea akupatia mafuta ya gari, vinjwaji au vitu kwa ajili ya vikao na mikutano” anasisitiza kiongozi huyo.
Your Ad Spot
Feb 28, 2025
Home
Unlabelled
JUMANNE ISMAIL MAKHANDA MWENYEKITI CCM WILAYA MANYONI AWAASA VIONGOZI
JUMANNE ISMAIL MAKHANDA MWENYEKITI CCM WILAYA MANYONI AWAASA VIONGOZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇