LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 24, 2025

DIWANI MLAGAZA WA MAKANDA MANYONI AMWAGA SIFA KWA RAIS SAMIA

 Na Dkt Dismas LYASSA, Manyoni


Diwani wa Kata ya Makanda katika Jimbo la Manyoni Mashariki, ndugu Jumanne Mlagaza, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya za kuharakisha maendeleo katika kata yake na Tanzania kwa ujumla.\

Akionyesha shule mpya zilizojengwa kwa jitihada za Rais Samia, Diwani huyo anasema kwa kweli anakosa la kusema zaidi ya kumshukuru sana Mungu kwa kutuletea Rais Dk Samia.

"Hapa Shule ilishaanza kubomoka kwa vile ilijengwa muda mrefu, tunamshukuru sana Rais ameliona hilo na sasa tuna madarasa mengi mapya na choo cha kisasa," anasema Diwani huyo.

Mlagaza anasisitiza kuwa kata yake licha ya kuwa ndani sana, lakini hilo halikuwa shida kwa Serikali kwani iliweza kuona shida iliyokuwepo na hatua zimechukuliwa.

"Maendeleo ni mengi, ni suala la kumshukuru sana Rais na nashauri Watanzania wenzangu kwa pamoja tumpe tena miaka mingine ya kuongoza ili atusaidie kuleta maendeo zaidi," anasema.

Kwa mujibu wa Diwani Mlagaza maendeleo yamepatikana karibu kila kona ikiwamo miundo mbinu huku pia jitihada mbalimbali zikiendelea kwa vile ambazo bado zipo.


Hali ilivyokuwa kabla ya ujenzi wa madarasa mapya (Picha na Vikta Makinda)

Ndugu Mlagaza alionyesha mojawapo ya madarasa mapya yaliyojengwa (Picha na Vikta Makinda)


 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages