Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma imepongeza serikali kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo kukamilisha Mradi wa Maji unaohudumia wakazi zaidi 9000 katika vijiji vya Mtego wa Noti na Mwangaza wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.
Mradi huo ambao umegharimu Shilingi 952, 610, 674 fedha za ufadhili kutoka mfuko wa pou Due Jenson, Groundfos foundation huku wananchi wakichangia Shilingi 47,630,534, umetekelezwa kwa lengo la kuwaondolea wananchi adha ya kutumia muda mwingi kufuata huduma ya maji yasiyo salama katika mabwawa na visima.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Jamal Tamimu amewapongeza wahisani wa mradi huo mfuko wa pou Due Jenson, Groundfos foundation kupitia shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kutekelezwa na shirka la Watermission na kwamba Chama kinathamini mchango wa Sekta binafsi katika maendeleo ya wananchi.
Katika hatua nyingine Tamim amesisitiza ukamilishwaji wa Miradi ya Maendeleo kwenda sambamba na utoaji wa Huduma kwa wananchi ili kuondoa adha zilizopo na kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.
Aidha, amewataka wananchi wilayani humo kuchangamkia fursa za maboresho ya Miundombinu ya barabara kwa kusafirisha bidhaa mbalimbali za kibishara ikiwemo mazao na kuyafikia masoko kwa wakati.
"Lengo moja wapo la serikali katika kuimarisha barabara katika maeneo ya vijijini ni kuwarahisishia wakulima kusafirishaji wa mazao na kuyafikia masoko kwa urahisi, hii italeta maana katika malengo ya serikali ya kukifanya kilimo kuwa biashara" amesema Tamim.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇