LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 9, 2025

MWANYIKA AMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAPATIA GARI LA WAGONJWA KITUO CHA AFYA UHALULA

MWANYIKA AMPONGEZ


Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa vituo vya Afya katika jimbo la Njombe Mjini vikiwemo vilivyokamilika na vinavyoendelea kujengwa pamoja na kutoa vifaa tiba, kuleta wataalamu na sasa wamepokea gari la wagonjwa la 3 kwa ajili ya kituo cha Afya Ihalula, awali alitoa magari ya wagonjwa katika vituo vya Afya Kifanya na Makowo .



Akizungumza katika hafla ya kukabidhi gari hilo, Mbunge Mwanyika amewataka wananchi kuitumia na kuitunza gari hiyo. Kupatikana kwa gari hilo la wagonjwa katika kituo hicho kutasaidia wananchi wa kata ya Utalingolo pamoja na maeneo jirani katika kupata huduma za dharura zinazohitaji gari ya wagonjwa ili kufikishwa katika hospitali kubwa kwa huduma zaidi.


Pia amewataka wataalamu wa Afya kuwa wavumilivu kufanya kazi katika mazingira ambayo serikali bado haijawa na nyumba za kutosha kwa ajili ya watumishi katika maeneo mbalimbali.


#Aliahidi, ametekeleza

#Njombe mpya

#Dira Mpya, kazi iendelee



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages