Ziara hiyo itajumuisha ushiriki wa Balozi Nchimbi katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Prosperity Party, pamoja na juhudi za kuimarisha uhusiano kati ya Ethiopia na Tanzania kupitia vyama hivyo viwili vinavyoongoza Serikali katika nchi hizo.
Vilevile, ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa diplomasia ya uchumi kati ya Ethiopia na Tanzania, uhusiano ambao ulijengwa miaka mingi iliyopita kwa misingi imara ya kisiasa wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika.
Mazungumzo kati ya Balozi Nchimbi na viongozi waandamizi wa Prosperity Party yataangazia mikakati ya maendeleo yenye manufaa kwa pande zote, hususan katika sekta za uwekezaji, biashara, ufugaji na teknolojia.
Balozi Nchimbi anatarajiwa kurejea nchini tarehe 1 Februari 2025.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇