KWA lengo la kuhakikisha usalama wa watalii na kurahisisha huduma, Serikali imewekeza kwenye teknolojia ya kisasa ya matumizi ya‘smart gates’ na ufungaji wa ‘CCTV cameras’ kwenye baadhi ya malango ya kuingilia, kutokea wageni na maeneo mengine muhimu ili kuboresha ukusanyaji wa mapato.
Aidha, Serikali ya Awmu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imeanza mchakato wa kujenga barabara kuu zinazotumika zaidi katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa kiwango cha tabaka gumu ili kupunguza athari za mazingira,kuboresha huduma kwa watalii na kupunguza gharama za matengenezo ya mara kwa mara.Hayo yamesemwa hivi karibuni na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumu, Morogoro, kuhusu masuala mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇