LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 6, 2024

WABUNGE WAPATA AJALI WAKISAFIRI KWENDA KWENYE MASHINDANO YA MABUNGE MOMBASA, BAADHI WAJERUHIWA

Dodoma, leo

Baadhi ya wabunge waliokuwa wanasafiri kwa basi la mabasi ya Shabiby kwenda Mombasa, Kenya kwenye mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Mombasa wamepata ajali eneo la Mbande Dodoma, baada ya basi lao moja kugonga na lori kwa nyuma, lililokuwa limesimama katika barabara ya Morogoro, leo alfajiri.

"Aisee, mambo siyo mazuri, basi moja kati ya manne tuliyokuwa tunasafiria limepata ajali na baadhi ya wenzetu wamejeruhiwa na kuwahishwa hospitali za Uhuru na Benjamini Mkapa kwa ajili ya matibabu, hatujui hadi sasa wenzetu wanaendeleaje, nasi bado tupo eneo la ajali," amesema kwa simu mbunge mmojawapo aliyekuwa katika msafara huo.

Msafara huo  ambao ulitakiwa kupitia Chalinze na Tanga kwenda Mombasa, umejumuisha wabunge na watumishi wa Bunge zaidi ya 120 wanaokwenda kushiriki michezo mbalimbali inayotarajia kuanza kesho Desemba 7 hadi Desemba 17 mwaka huu na kushirikisha timu za mabunge  ya Nchi 7 likiwemo Bunge la Afrika Mashariki.

Mtandao huu umefanya jitihada za kumtafuta kwa njia ya simu Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi, DCP, David Misime amepatikana na kuahidi kuifatilia ajali hiyo na kutoa uthibitisho baadaye.


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages