Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameazimia kuunda Tume mbili ambapo moja itachunguza na kutoa mapendakezo kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro. Tume nyingine itaangalia utekelezaji wa zoezi zima la uhamiaji kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo Ikulu ndogo ya Arusha wakati akizungumza na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai (Malaigwanani) wanaoishi katika eneo la Ngorongoro.
Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kuwasikiliza viongozi hao kufuatia kuwepo kwa malalamiko dhidi ya baadhi ya maamuzi ya Serikali yanayohusu eneo la Ngorongoro.
Rais Dkt. Samia amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuimarisha utendaji kazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimasai (Malaigwanani) wanaoishi Ngorongoro mara baada ya kikao kilichofanyika Ikulu ndogo ya Arusha tarehe 01 Desemba, 2024.
Baadhi ya jamii ya masai wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya mawaziri walioshiriki mazungumzo hayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇