LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 7, 2024

RAIS RUTO ATOA POLE KWA BUNGE LA TANZANIA KWA AJALI YA WABUNGE

 Rais wa Kenya, Mheshimiwa William Ruto ametoa pole kwa Bunge la Tanzania kwa ajali ya basi iliyowahusisha Waheshimiwa Wabunge wakati wakielekea Mombasa Nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Mheshimiwa Ruto ametoa pole hizo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo yanayoanza leo Desemba 6 hadi 17 Jijini Mombasa.

 

“Napenda nichukue fursa hii kutoa pole kwa marafiki zetu wa Tanzania kwa ajali iliyotokea, tunawatakia heri wote walioapata maumivu na majeraha na tunamuomba Mungu awape afueni.” Alisema.

 

Mheshimiwa Ruto pia pamoja na mambo mengine alihimiza umuhimu wa Utengamano wa Afrika Mashariki katika kuchochea maendeleo ya nchi wananchama na kwamba kupitia michezo hiyo  umoja unadumishwa.

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bunge Sport Club, Mheshimiwa Abbas Tarimba alisema licha ya baadhi wa wachezaji wa Timu ya Bunge kujeruhiwa katika ajali ya gari wapo tayari kushindana kikamilifu.

 

“Pamoja na ajali ambayo wenzetu 17 wamepata majeraha Tanzania tumeamua kuja kushindana, tumejiaandaa na tutaonyesha ushindani,” alisema.

 

Moja ya basi lililokuwa limewabeba Waheshimiwa wabunge kuja Mombasa nchini Kenya kushiriki katika mashindanoi haya lilipata ajali ya kugongana na lori la mizigo maeneo ya Mbande Dodoma.

 

Timu kutoka Bunge la Tanzania litashiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, kuvuta Kamba, vishale, riadha na gofu.

 

Mechi ya ufunguzi wa mashindano haya ya mpira wa miguu inachezwa  kati wenyeji Timu ya Bunge la Kenya na Timu ya Bunge la Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Mbaraki mjini Mombasa.


Rais wa Kenya, William Ruto ametoa pole kwa Bunge la Tanzania kwa ajali ya basi iliyowahusisha Wabunge wakati wakielekea Mombasa Nchini Kenya.
Timu ya Bunge wakiwa kwenye ufunguzi wa mashindano hayo.





 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages